Friday, December 5, 2025
Home > Counties > Busia > Wanaume waombwa kuwa msitari wa mbele kwa maswala ya hedhi

Wanaume waombwa kuwa msitari wa mbele kwa maswala ya hedhi

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya afya wakati wa hedhi miongoni mwa wasichana na wanawake, wito umetolewa kwa wanaume kujitenga na dhana potovu na badala yake wawe katika mstari wa mbele kuhakikisha wasichana na wanawake wanahudumiwa vilivyo wakati wao wa hedhi.

Wito huu umetolewa na Naibu Gavana wa Busia Arthur Odera na MCA wa Chakol kusini Dalmas Onjole, ambao wametoa changamoto kwa wazazi wa kiume kuwapa mazingira salama wanao na wake zao wakati wako kwenye hedhi kwa kuwanunulia vifaa hitajika.

“Maswala ya hedhi yasiwe ni siri tena, jamii yote yafaa jumuika kuhakikisha afya ya mtoto wa kike. Dunguzanguni tupuzilie mbali dhana potovu kwenye swala hili,” Naibu gavana Odera alisema.

Washikadau hao wametoa wito kwa serikali kurahisisha namna ya upatikanaji wa taulo za hedhi ili kuhakikisha wasichana wengi ambao hawana uwezo wa kupata sodo hawataabiki wakati wa hedhi.

Wadau mbali mbali wakiongozwa na Sarah Martha, mkurugenzi wa shirika la Dhamira moja na msaidizi wa kamishina Teso kusini Leo Stanley Amimo waliozungumza katika shule ya msingi ya Aterait eneo bunge la Teso kusini, wamesema kukosekana kwa taulo za hedhi kumechangia wasichana wadogo kutumbukia kwenye jinamizi la mimba za utotoni, wengine wakikatiza masomo yao.

“Watoto wengi wanaendelea kukosa shule kwa haya ya kukosa sodo; ni muhimu kila shule na soko kuwa saduku maalumu ya sodo ili kuwapa fursa kina mama na wasichana kutokuwa na uonga wa kuendeleza shugli zao,” Sarah Martha.

Idara ya afya kaunti ya Busia ikiongozwa na afisa mkuu katika idara ya afya ya jamii Dakt Susan Outa, imetoa changamoto kwa wizara ya elimu kuhakikisha kuwa wanafunzi wa kike wanapata mazingira salama ya kujistiri wakati wa hedhi.

Washikadau mbali mbali kutoka kaunti ya Busia wametoa wito kwa wanaume wote kuhakikisha kuwa wanawasaidia wanawake wakati wako kwenye hedhi na viongozi wote wahakikishe wasichana wote wanapata sodo wakati unaofaa na Kwa urahisi.

Idara ya afya imechukuwa jukumu la kuhakikisha kuwa kila choo ambacho kinajengwa kiko na chumba cha kubadilisha sodo. Pia idara hii imetoa onyo kwa watu ambao wana imani duni kuhusu hedhi.

Kwa mfano, visa vya matumizi ya karatasi, matawi na viraka wakati wasichana wako kwenye hedhi ni jambo ambalo limeendelea kuwa donda sugu. Kwa hivyo serikali imeombwa kuhakikisha kuwa wasichana pamoja na Watoto wote wanapata sodo wakati unaofaa.

Wazazi wameombwa kujukumika si tu kwa kulipa karo bali kwa kuhakikisha kuwa wasichana wao wanapata mazingira tulivu wakati wako kwenye hedhi. Kwa hivyo washikadau hawa waliwaomba wazazi waweze kuchukua jukumu ya kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata sodo wakati mwafaka.

Na Centrine Atenge

Leave a Reply