Home > Counties > Bungoma > Balozi wa Marekani azuru Bungoma

Balozi wa Marekani azuru Bungoma

Serikali ya Marekani inaunga mkono mchakato wa upatanishi wa BBI ili kuzipa serikali za kaunti mamlaka zaidi kupitia ugatuzi.

Haya yalisemwa na Balozi wa Marekani nchini Kenya, Kyle McCarter, alipozuru kaunti ya Bungoma mnamo Jumatatu, kutathmini miradi iliyozinduliwa na serikali ya hiyo ya ugatuzi, chini ya ufadhili wa serikali yake.

McCarter ambaye aliandamana na mkewe, alisema mpango wa upatanishi wa BBI haupaswi kubadilishwa na kuwa mbinu ya kwanufaisha wanasiasa, bali unafaa kuyatilia maanani matakwa ya wakenya wote.

Aidha serikali ya Marekani imetangaza kupiga jeki mpango wa kuimarisha elimu ya kiufundi nchini kupitia vyuo vya anuwai, mpango ambao unaendelezwa na serikali kuu ya kitaifa na zile za kaunti.

Kwa upande wake, gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati ameahidi kuwa Baraza la Magavana nchini litahakikisha kuwa mjadala wo wote kuhusu mpango wa BBI unaafiki malengo ya kuimarisha ugatuzi.

Wakati huo huo, serikali ya Marekani kupitia ubalozi wake humu nchini inatathmini miradi inayotekelezwa kupitia ufadhili wake, ikiwemo sekta ya afya katika kaunti zote 47 nchini.

Na  Fahima Hanisi/ Roseland Lumwamu

Leave a Reply