Sunday, April 21, 2024
Home > Editor's Pick > Oparanya ahidi Kuinua hadhi ya mji wa Kakamega

Oparanya ahidi Kuinua hadhi ya mji wa Kakamega

Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya amesema kwamba atafanya kila jitihada kuhakikisha mji wa Kakamega unapata hadhi ya jiji ifikapo 2022.
Oparanya alisema kuafikia hadhi hiyo kutawezesha mji huo kuvutia waekezaji wakubwa ndiposa uchumi wa kaunti uinuke na wenyeji wapate ajira.
Alisema hayo alipokuwa akitoa msaada wa chakula, blanketi, mafuta ya kupika, unga wa mahindi, sukari na bidhaa zingine kwa wakazi na vituo vya wasiobahatika ili nao waweze kusherehekea Krismasi.
Kiongozi huyu amesifiwa na wengi kwa kuafikia maendeleo makubwa katika sekta mbali mbali zikiwemo barabara na miundo msingi kwa jumla.
Miradi hiyo ni pamoja na kuinua uwanja wa michezo wa Bukhungu kuafikia kiwango cha kitaifa, ujenzi wa hospitali ya mafunzo na rufaa ambayo awamu ya kwanza imekamilika na kufadhili masomo ya chekechea katika shule za umma.
Aliwarai wakazi kutimiza upendo na amani msimu huu wa sherehe.
Na Sammy Mwibanda

Leave a Reply