Friday, May 24, 2024
Home > Counties > Bungoma > Wakazi kukata kiu kutoka mradi wa maji wa mlima Elgon

Wakazi kukata kiu kutoka mradi wa maji wa mlima Elgon

Gavana Kenneth Lusaka pamoja na Naibu wake, Jenepher Mbatiany hapo jana adhuhuri wamekagua mradi wa maji wa Chebyuk-Kibabii katika Mlima Elgon.

Takriban wakazi 100,000 wa kaunti ndogo za Mlima Elgon, Kabuchai na Kanduyi wataunganishwa kwa maji salama ya kunywa hivi karibuni, mradi huo ukamilikapo.

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika kufikia Agosti mwaka huu na unahusu usanifu wa mpango wa maji wa kaunti, ujenzi wa kituo cha kutibu maji hayo, kituo cha kukusanya maji hayo 600m3 kwa siku, njia ya usambazaji yenye Kilomita 7, matanki 4 ya kuhifadhi maji na maduka 25 katika Mlima Elgon, kaunti ndogo za Kabuchai na Kanduyi.

Akizungumza kwa niaba ya jamii, Jacklyn Chemutai alipongeza mradi huo akisema utatoa suluhu la kudumu kwa wakaazi wa Mlima Elgon ambapo changamoto ya maji ambapo eneo hilo limekuwa likishuhudia kwa muda mrefu.

Vile vile Lusaka ameidhinisha uboreshaji wa barabara ya Kipsgon – Kubura – Kapkerwa kama sehemu moja ya ajenda yake.

Eneo hilo la Kilomita 7 litanufaisha mamia ya wakaazi wa Mlima Elgon kwa uwekezaji na kuunganisha wadi ya Chebyuk na kaunti nzima ya Bungoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Gavana Lusaka amesema kuwa ameweka mikakati ya kuhakikisha kuwa barabara zote zinadumishwa mara kwa mara na kwamba serikali ya kaunti itamlipa mwanakandarasi kwa kazi Bora.

Lusaka aidha amesema kwamba baada ya kukamilika kwa barabara hiyo wakaazi wa eneo hilo watachukua muda mfupi kutoka Kapkerwa hadi Kipsgon.

Gavana aliandamana na Naibu Gavana Jenepher Mbatiany, waziri wa barabara Jimbo la Bungoma Bonventure Chengeck, wawakilishi wadi wa eneo Bunge la mlima Elgon na Maafisa Wakuu, katika serikali ya kaunti.

Na Douglas Mudambo

 

Leave a Reply