Tuesday, February 7, 2023
Home > Counties > Wakaazi wa Mtaa wa Lurambi Walalamikia Ukosefu wa Usalama

Wakaazi wa Mtaa wa Lurambi Walalamikia Ukosefu wa Usalama

Wakaazi wa mtaa wa Lurambi mjini Kakamega wameomba vyombo vya usalama kuimarisha hali ya usalama katika eneo hilo wakati wa usiku.

Inaarifiwa kwamba genge la vijana huvamia watu kwa mawe na mapanga kuanzia mwendo wa saa mbili usiku wanapoelekea nyumbani.

Mmoja wa waathiriwa Leonard Khakai alisema kwamba katika kipindi cha wiki moja iliyopita, zaidi ya watu watano wamevamiwa na kuachwa na majeraha mabaya vichwani.

Maeneo ambayo yameathiriwa ni pamoja na Koromatangi, Lurambi, Tea Zone na Sichirayi.

Afisa wa polisi anayesimamia kituo kimoja eneo hilo ambaye hakutaka kutajwa alisema wamepokea malalamishi na watashika doria kuhakikisha usalama umeimarishwa.

Usimamizi wa chuo kikuu cha Masinde Muliro umetoa tahadhari kwa wanafunzi wake dhidi ya kutembea usiku katika maeneo hayo.

Na Sharon Nasipondi, Sammy Mwibanda

Leave a Reply