Wednesday, February 8, 2023
Home > Education > Mwakilishi wadi amushukuru Ottichilo kwa kuboresha miundo misingi

Mwakilishi wadi amushukuru Ottichilo kwa kuboresha miundo misingi

Mwakilishi  wadi  katika bunge la Vihiga, Bi. Violet  Bagada ameishukuru serikali ya gatuzi la Vihiga kwa uzindushi wa shughuli  ya kuboresha miundo misingi katika chuo cha anuwai cha Keveya.

Bagada  alitoa shukurani hiyo Jumamosi alipozuru chuo hicho kilicho katika gatuzi ndogo la Sabatia.

“Uboreshaji  wa miundo misingi katika vyuo vya anuwai katika gatuzi letu kutachangia pakubwa sana katika kiwango cha masomo ya wanafunzi wetu,” alisema Bagada.

Mwakilishi  wadi huyo aliorodhesha ukosefu wa madarasa ya kutosha, maktaba, mabweni na vyoo kuwa miongoni mwa changamoto  ambazo vyuo vya ufundi vinakumbana nazo katika sehemu hiyo.

Hata hivyo, Bagada  alimshukuru Gavana  Willber  Ottichilo kwa kile alichokitaja kama usimamizi bora wa fedha na rasilimali ya  gatuzi laVihiga.

“Tangu  Gavana Ottichilo  achukue hatamu ya uongozi tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika matumizi ya fedha za serikali  ikilinganishwa na serikali ya hapo awali,” alikariri Bagada, huku akiwarai wenyeji kumpatia Ottichilo muda wa kutekeleza  manifesto yake.

Mwana  siasa huyo, alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanafunzi katika chuo cha Keveye kusoma kwa bidii ili wahitimu na ujuzi  utakaosaidia kuboresha hali ya kiuchumi na maendeleo katika gatuzi la Vihiga.

Siku  ya  alhamisi Gavana Ottichilo alikabidhi chuo hicho hundi ya shs.7, 800, 000 kwa wanafunzi 520 ambapo kila mwanafunzi  alilipiwa karo ya sh.15, 000 na serikali ya gatuzi hilo.

Aidha gavana huyo alizindu rasmi shughuli ya ujenzi wa madarasa ya kisasa katika chuo hicho.

Na  Wachira  Josphat

Leave a Reply