Home > Counties > Washukiwa wa ujambazi wauawa na polisi Ikolomani

Washukiwa wa ujambazi wauawa na polisi Ikolomani

Washukiwa watano wa ujambazi wamepigwa risasi na kuaga papo hapo baada ya makabiliano kuzuka baina yao na maafisa wa kitengo maalum (special unit) eneo la Makhokho katika barabara ya Kakamega kuelekea Kisumu.

Inaarifiwa kuwa watano hao waliokuwa wameabiri gari ndogo walikuwa wakifuatwa na maafisa wa polisi na punde kufiatuliana risasi kukaanza.

Kinara wa polisi eneo la Ikolomani Joseph Chesire amesema washukiwa walipatikana na bastola, risasi, sare rasmi za polisi miongoni mwa vifaa vingine.

Wakazi walioshuhudia kisa hicho cha kufiatuliana risasi wamewataka maafisa wa polisi kuendeleza msako dhidi ya wahalifu katika eneo hilo.

Na Sammy Mwibanda

Leave a Reply