Home > Editor's Pick > Mtahiniwa ajifungua mapacha

Mtahiniwa ajifungua mapacha

Huku  mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne ukianza Jumatatu, mwanafunzi mmoja amelazimika kuufanya mtihani huo hospitalini baada ya kujifungua mapacha usiku wa kuamkia leo.

Mwanafunzi huyo kutoka shule moja ya upili katika kaunti ndogo ya Marakwet Magharibi, alikimbizwa hospitalini hapo jana na kufanikiwa kujifungua bila matatizo yoyote.

Mkurugenzi wa elimu katika eneo hilo, Evans Onyancha alisema alitembelea mwanafunzi huyo katika hospitali ya kimisheni ya Kapsowar kuona kwamba anaendelea na mtihani wake bila shida yoyote.

“Tuliweza kumpelekea mtihani na pia kutoa msimamizi na askari ambao wote ni wanawake huko hospitalini kumwezesha kuendelea na mtihani wake,” alisema Onyancha.

Mkurugenzi huyo alilalamikia ongezeko la wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni na kusema kwamba yeyote atakayepatikana amehusika atachukuliwa hatua kali.

Na  Alice  Wanjiru

Leave a Reply